02Nov 2018

UTATHIMINI WA MAUDHUI KATIKA TAMTHILIA ZILIZOTEULIWA KUTAHINIWA KATIKA SHULE ZA UPILI NCHINI KENYA: MSTAHIKI MEYA (2009) NA KIGOGO (2016).

Crossref Cited-by Linking logo
  • Abstract
  • Keywords
  • References
  • Cite This Article as
  • Corresponding Author

Utafiti huu unalenga kutathmini uhalisia wa maudhui katika tamthilia zilizoteuliwa kitahiniwa katika shule za upili hususan tamthilia ya mstahiki meya (Arege, T. 2009) na Kigogo (Kea, P. 2016). Katika kuzisoma tamthilia hizi na kuzitathmini tamthilia hizi, ni kweli kuwa tamthilia hizi zina ukaribiano wa kimaudhui lakini je kazi hizi za tamthilia zilihahakisi uhalisia wa mambo katika jamii kipindi ambacho ziliteuliwa kutahiniwa? Hata hivyo mtafiti alijiuliza kuwa je, ni kigezo kipi kinatumiwa kuteuwa tamthilia hizi kuwa za kutahiniwa katika kipindi Fulani ilhali zafanana kimaudhui? Je ni hali halisi ya kimaisha katika jamii wakati wa kuteua kazi hizi? Ikiwa ni hivyo,mtafit anatarajia kuzichunguza tamthilia hizi ili kubainihali ya uhalisia wa kijamii wakati katika kpindi cha kuteuliwa tamthilia hizi ili kubaini ufaafu wake kwa wanafunzi ambao ni kiwakilishi cha jamii kwa wakati ule.Utafiti huu utatathmini maudhui katika tamthilia hizi na kuonyesha umuhimu wake kwa wanafunzi na uhalisia wake katika jamii katika kipindi cha kuteuliwa kwake.Tutauchanganua maudhui katika kazi hizi mbili mintaaarafu matukio na hali halisi za kijamii na kuzitathmini tukitumia nadharia ya uhalisia. Kwa kutumia msingi ya nadharia ya Uhalisia ili kufikia maamuzi ya kuwa ama maudhui ya tamthilia hizi yalifaa kwa kipindi cha kuteuliwa au la. Mtafiti atapendekeza njia mwafaka za kuteua kazi za fasihi za kutahiniwa kwa kurejelea matokeo ya utafiti wetu.Ili kufikia malengo yetu, utafiti utazichanganua tamthilia hizi kwa undani na tutarejelea matukio halisi kama yalivyoripotiwa katika vyombo vya habari, kusakura kwenye mitandao kubaini masuala halisi jamii kama vile ; maudhui ya kisiasa, mungawanyiko wa jamii kwa mipaka ya kijamii, chuki, ukabila miongoni mwa mambo mengine yanayoiadhiri jamii ya leo na kisha kutathmini kwa kutumia nadharia teule ya uhalisia ili kubaini iwapo tamthilia ambazo zinateuliwa zinalenga mambo yale kwa kuangalia maudhui makuu ya tamthilia ya Mstahiki Meya(2009)na Kigogo(2016).Ni bayana kwamba mengi ya kuhusu maudhui yamefanywa katika tamthilia hizi hasa ikichukuliwa kwamba ni kazi ambazo zimetahiniwa katika shule za shule za upili katika vipindi tofauti. Hata hiyo utafiti huu unaegea zaidi kwa maudhui makuu ya kazi hizi ,kuyatathimini na na kuyaoanisha na mambo halisi katika jamii katika vipindi hivi vya utahini lengo kuu likiwa kuchunguza uhalisia wa maudhui makuu katika jamii na umuhimu wake kwa wanafunzi katika vipindi vile. Utafiti huu una sehemu tatu: sura ya kwanza inahusisha : suala la utafiti , maswali ya utafiti,malengo ya utafiti, mihili ya nadharia, sababu za kuchagua mada , upeo na mipaka na uteuzi wa data na uwasilishaji hata. Sura ya pili itashughulikia historia fupi ya waandishi wa tamthilia za Mstahiki Meya (2009)na kigogo(2016), udurusu wa maandishi ya watafiti wengine ili kupata maoni yao kuujenga utafiti huu.Sura ya tatu itahusiana na mbinu za utafiti pamoja na zile za uchanganuzi wa data. Katika kukusanya data, utafiti huu utatumia mbinu ya kusoma makala maktabani na kusakura katika mitandao.sura ya nne ni sehemu ya uchanganuzi wa data iliyokusanywa kutoka kwa tamthilia teule na majibu ya hojaji za walimu na wanafunzi.sura ya tano ni ya muhutasari wa matokeo, hitimisho na mapendekezo.


  1. Ambrose K. Ngesa, Enock Matundura na John Kobia (2015) Mwingiliano wa matini katika tamthilia za Kiswahili: Mashetani na Kijiba cha moyo.
  2. Arege, T. M. (2009). Mstahiki Meya. Nairobi: Vide-Muwa Publishers Ltd.
  3. Chacha, N. C. (1980). Ushairi wa Abdilatif: Utenzi wa Maisha ya Adamu na Hawaa (1971)
  4. 33Chimera, R. na Njogu, K. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
  5. Fridah G. O. (2017) Uhakiki Wa Mtindo Katika Tamthilia Za AregeTasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Maasai Mara. (Haijachapishwa)
  6. Kamusi ya Karne ya Ishirini na Moja (2011). Toleo la pili. Nairobi: Longhorn Publishers.
  7. Katutu, R. (2013). Mtindo katika Diwani ya Mfuko Mtupu na Hadithi Nyingine. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi (Isiyochapishwa).
  8. Kaui, T (2008) usawiri wa vijana katika tamthilia teule zaKiswahili WakatiUkuta (1971) na Uasi (1980). Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
  9. Kea, P. (2016).Kigogo.Nairobi.story Moja publishers.Ltd.
  10. Kinara, G. (2012) ?Maudhui ya Ukimwi Katika Riwaya za Kiswahili?. Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
  11. Kitula, K. N.W. (2012). Mwongozo wa Mstahiki Meya. Nairobi: Target Publications Ltd.
  12. Kothari, C. K. (1990). Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: Wiley.
  13. Mugambi, E. K. (1983) ?Kilio cha Wanyonge katika Riwaya za Mohamed, S.A?. Tasnifu ya uzamili, Chuo kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa)
  14. Muthoni, M. (2014). Uhakiki wa Maudhui na Mtindo katika Tikitimaji. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi (haichapishwa).
  15. Mwanakombo, M. M. (1994). Uchambuzi wa dhamira, falsafa na mitindo katika tamthilia mbili za Chacha N. Chacha. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Moi (Isiyochapishwa).
  16. Mwita, S. M. (1994). Tamthilia mbili za Ebrahim Hussein: Arusi na Kwenye Ukingo wa Thim. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Moi (haichapishwa).
  17. Ng?etich, B. (2011) ?Dini kama Chombo cha Kuwadhulumu Waumini?. Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu Cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
  18. Ngolo, E. K. (2011). Mabadiliko ya Kimtindo katika Ushairi wa Said A. Mohamed. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta (haijochapishwa).
  19. Ngonyani, D. (2005). Vitendawili vya Kiswahili: Usambamba wake na Dhima yake katika Jamii.‟ Katika Swahili Forum nambari 12, Uk.122-123. Chama cha Masomo ya Kiafrika.
  20. Njogu, K. (2007) Kiswahili na Elimu Nchini. Limuru: Kolbe Press
  21. Njogu, K. na Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
  22. Njoroge, A. W. (2014) ?Viongozi kama Visababishi vya Mabadiliko katika Riwaya za Mwenda Mbatiah: Vipanya vya Maabara na Majira ya Tufani?. Tasnifu ya uzamili, Chuo kikuu Cha Nairobi (Haijachapishwa).
 

[Muthui Evelyn Kakivi and Esther Njoki Chomba. (2018); UTATHIMINI WA MAUDHUI KATIKA TAMTHILIA ZILIZOTEULIWA KUTAHINIWA KATIKA SHULE ZA UPILI NCHINI KENYA: MSTAHIKI MEYA (2009) NA KIGOGO (2016). Int. J. of Adv. Res. 6 (Nov). 130-137] (ISSN 2320-5407). www.journalijar.com


DR.ESTHER NJOKI CHOMBA
SUPERVISOR

DOI:


Article DOI: 10.21474/IJAR01/7979      
DOI URL: http://dx.doi.org/10.21474/IJAR01/7979