31Aug 2016

MATUMIZI YA VISAIDIZI VYA UFUNDISHAJI MSAMIATI WA KISWAHILI KATIKA SHULE ZA MSINGI ZA UMMA, KAUNTI YA KISUMU MASHARIKI, KENYA.

  • Kenyatta University, School of Education, P. O. Box 43844, Nairobi, Kenya.
Crossref Cited-by Linking logo
  • Abstract
  • Keywords
  • Cite This Article as
  • Corresponding Author

Utafiti huu ulishughulikia uchunguzi wa matumizi ya vifaa vya ufundishaji wa msamiati wa kiswahili katika shule za msingi za umma, Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki, Kenya. Malengo aliyozingatia mtafiti katika utafiti huu yalikuwa pamoja na kutambua changamoto zilizopo wakati wa kutumia vinyago, video na chati katika somo la msamiati, kudadisi sera zilizopo za ukaguzi ili kudhibiti utumizi wa video, chati na vinyago ili kusaidia uelewekaji wa msamiati na kuchunguza udhaifu na ufaafu uliopo katika ufundishaji msamiati kwa kutumia video, chati na vinyago katika somo la Kiswahili. Utafiti ulilenga idadi ya walimu kumi wa Kiswahili katika Shule za msingi katika Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki. Baadhi ya hizi mtafiti aliteuwa kwa bahati nasibu walengwa walioteuliwa kama hivi walimu wakuu kumi, walimu wa Kiswahili kumi na wanafunzi kumi. Walengwa wote walikuwa mia nane ishirini ambao waliimbua asilimia kumi, basi idadi ilio hojiwa ikawa themanini na wawili. Hojaji zilikuwa tatu za walimu wakuu, walimu wa Kiswahili. Utafiti ulichanganuliwa kwa kutumia SPSS kuonyesha idadi katika alama za asilimia na uradidi. Baada ya kutafiti na kuchanganua data, mtafiti alipendekeza haja ya walimu wa Kiswahili kuwa na vikao katika majopo. Mtafiti pia aona kuwa kuna haja washika dau wote wa elimu kufufua taasisi za Kaunti ili kukuza hitaji la uundaji visaidizi ili walimu wapate kuendeleze ueledi wao wa kuunda visaidizi ili kuboresha uelewekaji wa dhana za Kiswahili. Kadhalika, washika dau wana changamoto kubwa ya kuleta mashuleni rasilimali ya kutosha kutengeneza visaidizi vinavyohitajika. Jambo lingine ni kuwa shule zingetenga sehemu mahususi ya kuhifadhi visaidizi ili vitumike bila uwoga wa kuharibika ama kupotea. Mwisho, walimu watie misingi thabiti ya ufunzaji msamiati kuanzia madarasa ya chini ili wanafunzi wasielewe dhana hizi kimakosa kisha wahitajike kurekebishwa baadaye. Jambo hili ndilo lililokita mizizi sehemu nyingi za Kaunti ya Kisumu Mashariki, Kenya.


[Kamau Hellen Wambui, Samson Ondigi and Hamisi Babusa. (2016); MATUMIZI YA VISAIDIZI VYA UFUNDISHAJI MSAMIATI WA KISWAHILI KATIKA SHULE ZA MSINGI ZA UMMA, KAUNTI YA KISUMU MASHARIKI, KENYA. Int. J. of Adv. Res. 4 (Aug). 281-288] (ISSN 2320-5407). www.journalijar.com


KAMAU WAMBUI HELLEN


DOI:


Article DOI: 10.21474/IJAR01/1215      
DOI URL: http://dx.doi.org/10.21474/IJAR01/1215