02Sep 2019

UKOPAJI WA LUGHA: ETIMOLOJIA NA MABADILIKO YA MAANA NA UTAMKAJI WA MSAMIATI WA KIARABU KATIKA KISWAHILI.

  • Chuo Kikuu cha Kenyatta
Crossref Cited-by Linking logo
  • Abstract
  • References
  • Cite This Article as
  • Corresponding Author

Pindi wazungumzaji wa lugha mbili wanapotagusana na kuingiliana basi moja kwa moja lugha hizo huweza kukopana na kuathiriana kifonolojia, kimsamiati na kisarufi. Waarabu walipofika pwani ya Afrika Mashariki, walikumbana na Waswahili na hapo ndipo Kiswahili kikakopa maneno na sauti za kiarabu ambazo hazikuwepo katika lugha ya Kiswahili. Pili, Kiswahili pia kikachukua baadhi ya sauti za kiarabu na kuzibadili jinsi zinavyotamkwa. Makala haya yanatafiti na kuainisha etimolojia ya baadhi ya maneno ya kiarabu yanayopatikana katika lugha ya Kiswahili na jinsi sauti za kiarabu zilivyokopwa na kubadilishwa na kuswahilishwa.na pili namna baadhi ya maneno yalivyobadilishwa maana asilia baada ya kukopwa kutoka lugha ya Kiarabu. Nadharia za mfumo na semantiki tambuzi za msamiati zilitumika.


  1. Khamisi A. B. (2012) Kamusi Asisi ya Kiingereza-Kiswahili-Kiarabu; Dar es Salaam; Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI)
  2. Mulder J. & Hervey S.G. (1975) ?Language As a System of Systems? Linguistique, 11, 2, 3-22, 75
  3. OUP (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la Pili); Nairobi; Oxford University Press
  4. Paradis, C. (2012).\'Lexical Semantics\', In TheEncyclopaedia of Applied Linguistics (Ed.),Chappelle C. Oxford: Willey -Blackwell (pp.3347-3356).

[Hamisi Babusa. (2019); UKOPAJI WA LUGHA: ETIMOLOJIA NA MABADILIKO YA MAANA NA UTAMKAJI WA MSAMIATI WA KIARABU KATIKA KISWAHILI. Int. J. of Adv. Res. 7 (9). 101-105] (ISSN 2320-5407). www.journalijar.com


DR. HAMISI BABUSA
KENYATTA UNIVERSITY

DOI:


Article DOI: 10.21474/IJAR01/9635       DOI URL: http://dx.doi.org/10.21474/IJAR01/9635


Share this article