UREJELEOMATINI KATIKA UWASILISHAJI WA MAUDHUI YA DHULUMA KATIKA RIWAYA YA MSICHANA WA MBALAMWEZI (K.W.WAMITILA).
- Chuo Kikuu cha Egerton, Kenya.
- Chuo Kikuu cha Kabianga, Kenya.
71 Downloads
614 Views
Abstract
Waandishi wa riwaya ya Kiswahili ya kisasa wanawasilisha ujumbe kwa hadhira kwa kujikita katika mbinu za kiuandishi za kimajaribio. Urejeleomatini ni mojawapo wa vipengele muhimu vya mbinu hizo za kimajaribio. Riwaya zenyewe zimeitwa ?riwaya za kimajaribio? au ?riwaya za kisasa?. Watalaamu wengine wamezibaini kama ?riwaya za Karne ya Ishirini na Moja. Mwandishi Kyallo Wadi Wamitila ni mmojawapo wa waandishi wa kisasa anayetumia mtindo huu mpya wa kiuandishi katika kuzungumzia maswala mbalimbali yanayoikumba jamii. Nadharia ya usasaleo imeongoza utafiti huu katika uchanganuzi wakipengele cha urejeleomatini. Aina mbali mbali za matini zilizorejelewa katika uwasilishaji wa maudhui ya dhuluma zilitambulishwa na kufafanuliwa. Riwaya ya Msichana wa Mbalamwezi ilichaguliwa kimaksudi kwa kuwa inawasilishwa kwa simulizi nyingi fupi fupi zinazorejelea matini tofauti tofauti. Mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo mkabala wa kimaelezo ilitumika kuchanganua deta iliyohusiana na swala zima la urejeleomatini. Deta ilichanganuliwa kwa kuangazia maudhui, mandhari na mbinu za kiuandishi za kimajaribio. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Ilibainika kuwa ukosefu wa utaratibu katika uendeshaji wa mambo ndiyo taswira kamili ya jamii ya sasa. Matini zilizorejelewa zimeonyesha kuwa mwananchi amedhulumiwa na kupewa huduma duni na viongozi. Makala hii imehakiki na kutathmini jinsi mwandishi anavyotumia mbinu ya urejeleomatini kama kunga ya uwasilishaji wa maudhui ya dhuluma katika riwaya ya Msichana wa Mbalamwezi.
Keywords
How to Cite This Article
Janice M. Mutua, AbdulRahim Taib and Issa Mwamzandi. (2019); UREJELEOMATINI KATIKA UWASILISHAJI WA MAUDHUI YA DHULUMA KATIKA RIWAYA YA MSICHANA WA MBALAMWEZI (K.W.WAMITILA)., International Journal of Advanced Research (IJAR), 7 (05), 303-308, ISSN 2320-5407. DOI: https://doi.org/10.21474/IJAR01/9038
Corresponding Author
Article Analytics
References
- Abrams, M.H. (1993). The Norton Anthology to English Literature II. New York na London: W.W. Norton.
- Anderson, F.B., (2004). ?Intertexuality and Memory in Yizo Yizo. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg.
- Bakhtin, M. (1981). The Dialogic Imagination. Austin: University of Texas Press.
- Baudrillard, J. (1994). Simulacra and Simulations. Ann Arbor: Michigan University Press.
- Best, S. na Kellner D. (2001). The Postmodern Adventure.?London, England, na New York:?Routledge and Guilford Press.
- Carter, D. (2006). Literary Theory. Harpenden, Herts, AL5 IX: Pocket Essentials.
- Diegner, L. (2005). ?Intertexuality in Contemporary Swahili Novel: Euphrase Kezilahabi?s Nagona and William E. Mkufya?s Ziraili na Zirani in Swahili Forum 12 (2005): 25-35.
- Enani, M., (1996). Comparative Moments. Cairo: GEBO.
- Habermas, J. (1987). The Philosophical Discourse of Modernity. Twelve Lectures, translated by Frederick Lawrence. Cambridge: The MIT Press.
- Jilala, H. (2016). Misingi ya Fasihi Linganishi Nadharia, Mbinu na Matumizi. Dar es Salaam: Daud Publishing Company.
- Kamunde, M.E. (1983). ?Kilicho cha Wanyonge katika Riwaya za Said A. Mohammed?. Tasnifu ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Nairobi.
- Kristeva, J. (1980). Word, Dialogue and Novel. Desire in Language: A Semiotic Approach to Literature and Art. Ed. Leon S. Roudies. New York: Columbia University Press. 64-91.
- Kwambai, M.K. (2016). ?Walenisi? and ?Mafuta? Depiction of Class Segregation?. Journal of Literature, Languages and Linguistics Vol 26.
- Lyotard, J.F. (1984). The Postmodern Condition: A Report on Knowledge. Manchester: Manchester University Press.
- Mohammed, S.A. (1995). Kunga za Nathari ya Kiswahili. Tamthilia, Riwaya na Hadithi Fupi. Nairobi: East African Publishers.
- Mwamzandi I.Y. (2013). Riwaya Teule za Karne ya Ishirini na Moja na Udurusu wa Nadharia ya Fasihi. Swahili Forum 20 (2013): 48-66.
- Njogu, K., (1987). ?Maudhui ya Mapinduzi katika Riwaya za Visiwani Zanzibar?. Tasnifu ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Nairobi.
- Rettova, A. (2016). ?Writing in the Swing? Neo-realism in Post- Experimental Swahili Fiction?. Research in African Literatures, (47) 2, pp. 15-31
- Stam, R., (2000). Film Theory: An Introduction. Oxford: Blackwell.
- Wamitila, K.W. 2007). Narrative Structure and Metaphor: Towards a New Aesthetics of the Kiswahili Novel. KISWAHILI: 70: 67-752.
- Wamitila K.W. 2011). Msichana wa Mbalamwezi. Nairobi: Vide-Muwa Publishers.
- (2010). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: English Press.
This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.





